Mwenyekiti wa kitongoji ADC aomba ushirikiano

MWENYEKITI pekee wa kitongoji anayetokana na Chama cha ADC, Mtoro Bakari Mvunye ameomba watendaji wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya Kigoma kumpa ushirikiano ya kuwatumikia wananchi kwa mafanikio.
Mvunye ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwandiga Kaskazini kwenye mji mdogo wa Mwandiga halmashauri hiyo akiwa pia Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa wa Chama cha ADC amesema dhamira yake ni kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo kulingana na mipango ya serikali.
Akizungumza mbele ya Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo (CCM) Mkoa Kigoma, Deogratius Nsokolo aliyembetelea nyumbani kwake kumpongeza kwa ushindi huo mwenyekiti huyo amesema Diwani na diwani na mbunge wote ni CCM, hivyo kushirikiana na viongozi hao utamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio.
Akizungumza na mwenyekiti huyo wa kitongoji nyumbani kwake alipomtembelea Nsokolo alimpongeza mwenyekiti huyo pekee anayetokana na chama cha ADC kwa ushindi alioupata ambao unampa nafasi ya kuwatumikia wananchi.
Nsokolo alimuomba mwenyekiti huyo kuwa baada ya kushinda kiti hicho cha kitongoji anapaswa kufanya kazi na vyama vyote ikiwemo CCM kwa kuunda baraza la ushauri la vyama mchanganyiko kwani Pamoja na ushindi huo wapo pia wanachama wa CCM ambao ni wananchi wake na wengine mmoja mmoja walimpigia kura wakiona anafaa kuwaongoza.