Mwigulu aagiza watumishi Temesa wafutwe kazi

DAR ES SAALM; WAZIRI Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, ameagiza watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) waliohusika na ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh bilioni 2.5 wafukuzwe kazi mara moja, akisisitiza kuwa serikali haitavumilia matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.

Dk Mwigulu ametoa agizo hilo leo Desemba 24, 2025 alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa kivuko eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa vitendo vya ubadhirifu vimekuwa chanzo cha kudorora kwa huduma za usafiri wa vivuko na kuongeza gharama zisizo za lazima kwa serikali.

β€œWatu wasioweza kujirekebisha ni lazima warekebishwe. Kumekuwepo na matumizi mabaya ya madaraka na fedha, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa,” amesema Dk Mwigulu.

Amebainisha kuwa kwa sasa matengenezo yamesimama kwa baadhi ya vivuko kutokana na madeni ya takribani Sh milioni 800, huku taarifa za kifedha zikionesha baadhi ya watumishi wa TEMESA wamehusika na ubadhirifu wa Sh bilioni 2.5.

Dk. Mwigulu ameonya kuwa endapo hatua kali hazitachukuliwa, serikali inaweza kujikuta ikitumia fedha nyingi katika matengenezo ya vivuko chakavu badala ya kununua vivuko vipya, hali itakayoongeza mzigo kwa wananchi na kuathiri utoaji wa huduma.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. β˜…ε½‘[𝐍𝐄𝐄𝐃 ππ„πŽππ‹π„ π…πŽπ‘ 𝐏𝐀𝐑𝐓 π“πˆπŒπ„ πŽππ‹πˆππ„ π–πŽπ‘πŠ]ε½‘β˜…

    Start making cash right now… I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my befst friend earns over $19,000 a month doing this and she convinced me to try. ift was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by visiting Following Link…

    π‡πžπ«πž 𝐒𝐬 𝐈 𝐬𝐭𝐚𝐫𝐭𝐞𝐝=========> https://bs786s.blogspot.com/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button