Mwimbaji wa Injili Rwanda kutumbuiza Tanzania

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili kutokea nchini Rwanda, Israel Mboni anayetamba na wimbo wake wa ‘Nina Siri’ ametua nchini tayari Tanzania kutoa huduma katika tamasha la uimbaji.

Matamasha hayo yanayotarajia kufanyika Novemba 2 ukumbi wa Mlimani City na Novemba 3 mwaka huu katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema anafurahi kuja nchini Tanzania kufanya huduma na anawapenda sana watanzania.

Advertisement

“Nimekuja kutoa huduma ya uimbaji, tutaimba na kucheza pamoja watanzania na kufurahia wakati wa Mungu naamini watabarikiwa na kazi ya Mungu nitakayofanya, watu wajitokeze kwa wingi rafiki zangu waje kufurahia matendo makuu ya Mungu.

Muandaaji wa ibada hiyo ya kumsifu Mungu Lilian Mkumbo amewataka kujitokeza kwenye ibada ya wakati wa Mungu na kufurahia lakini pia amesema hadi sasa mwitikio nimzuri watanzania wamepokea kwa wingi.

Kwa upande wake Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Rehema Semfukwe amesema kuwa upendo walioonyesha watanzania kupokea katika uwanja wa ndege wajitokeze kwenye tamasha.

“Husipange kukosa Baraka hizi ni kubwa mno katika ibada njooeni tuimbe na tucheze kwa pamoja tumshukuru Mungu wote mnakaribishwa.