SMZ kuimarisha uchumi wa buluu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Rais Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya sekta ya Uchumi wa Buluu ili wananchi wananufaika zaidi na kuongeza kipato chao.

Akizungumza na wavuvi, wakulima wa mwani na wananchi katika Bandari ya Mkoani, Rais Mwinyi alisema sekta ya uvuvi na kilimo cha mwani ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa sera ya Uchumi wa Buluu.

Rais alisema Serikali ya Awamu ya Nane inaendelea kuwajengea uwezo wakulima na wavuvi kupitia utoaji wa vifaa vya kisasa, ujenzi wa masoko na madiko, pamoja na mafunzo ya kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao yao. “Jitihada hizi zimeanza kuzaa matunda. Tunaona ongezeko la mavuno ya mwani na kiwango cha samaki wanaovuliwa,” alisema Rais Mwinyi.

Aidha, alisema Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo diko na soko la Mkoani pamoja na kiwanda cha mwani cha Chamanangwe. Lengo ni kuwaandalia wakulima mazingira bora ya uzalishaji. SOMA: Mwinyi kuboresha bandari ya Shumba

Rais Mwinyi alisisitiza kuwa Serikali itaendeleza ujenzi wa miundombinu ya Uchumi wa Buluu katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba, ikiwemo Bandari ya Shumba, soko la Kiwani na kiwanda cha kusarifu mwani cha Chokocho.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button