Mwinyi: Tusipandishe bei za bidhaa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amewahimiza wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kufanya biashara kwa uadilifu na kuwa na Huruma kwa wananchi.
Alhaj Dk Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Masjid Jibril Mkunazini alipojumuika katika Sala ya Ijumaa.
Aidha Alhaj Dk Mwinyi amesema kumekuwa na kawaida na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei za bidhaa wakati huo.
Amefahamisha kuwa Serikali imekuwa ikipunguza ushuru katika Mwezi wa Ramadhani hivyo si jambo jema kwao kupandisha bei za bidhaa na kuwaongezea mzigo wananchi.
Akizungumzia suala la Uchaguzi Mkuu Ujao Alhaj Dkt, Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi Kudumisha Amani ili Uchaguzi huo Ufanyike kwa Utulivu na Amani.
Wakati huo huo Rais wa Zanzibar Alhaj Dk Mwinyi amefika Jamati la Jumuiya ya Ismailia Aga Khan Kiponda na kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Kiongozi wa Jumuiya hiyo Aga Khan wa Nne Prince Shah Karim Al- Hussein aliyefariki hivi karibuni mjini Lisbon, Ureno akiwa na miaka 88.
17 comments
  1. I’m truly enjoying the design and layout of your site.

    It’s a very easy on the eyes which makes it much more pleasant for me to come here and visit more
    often. Did you hire out a designer to create your theme? Outstanding work!

  2. It’s really a great and useful piece of information.
    I’m satisfied that you simply shared this useful information with us.
    Please stay us informed like this. Thank you for sharing.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *