Mzazi wa Fid Q afariki

MTANDAO: MWANAMUZIKI wa Hiphop nchini Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amefiwa na baba yake mzazi, Mzee Kubanda.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, @therelfidq ameandika “Ninasikitika kuwataarifu ya kwamba.. mzee wangu, baba yangu, Mzee Kubanda ametangulia mbele ya haki,”

Fid Q ameeleza kuwa mazishi ya babaye yatafanyika kesho kijijini kwake Nasa mkoani Mwanza.“Inna lillah wainna ilaih raajiuun 🙏🏾 (Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea).” Ameandika Msanii huyo.

Habari Zifananazo

Back to top button