Mzigo wa amani na utulivu: Namna Polisi ilivyobeba uzito wa utulivu wa taifa

SIKU kabla ya uchaguzi, wakati na baada ya uchaguzi mara chache huwa tulivu. Katika demokrasia, siku hizo huleta hofu, kauli za ushindani na kuibua hisia. Tanzania haikuachwa nyuma. Matukio yaliyoripotiwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 yaliviweka vyombo vya usalama katika shinikizo la kutuliza hofu huku likitelekeza misingi ya Katiba.

Tathmini ya matukio iliyofanywa kwa kuzingatia majukumu na uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, inaonesha hatua zilizoratibiwa kisasa kuliko pengine ilivyozoeleka panakuwapo na hali ya joto la kisiasa. Badala ya kutenda kwa msukumo, polisi wakati wa kipindi hiki waliongozwa na sheria, miongozo waliyojiwekea na kujikita katika kusisitiza kuzuia na kushirikiana na jamii.

Mamlaka ya Jeshi la Polisi Tanzania siyo isiyo rasmi au ya hiari. Iko kikatiba. Ibara ya 147 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaunda vyombo vya ulinzi na usalama, wakati Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Polisi na Huduma Saidizi,

Sura 322 (kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023), imefafanua majukumu ya polisi. Majukumu hayo ni pamoja na kulinda maisha ya watu na mali, kusimamia amani na utulivu, kusimamia utekelezaji wa sheria, kubaini na kuzuia uhalifu, kukamata watuhumiwa na kufanya uchunguzi.

Kimsingi, utaratibu huo wa kisheria pia unabainisha ukomo wa madaraka ya polisi na kuweka mifumo ya uwajibikaji. Wakati wa nyakati tete za kisiasa, taratibu hizi zinaondoa ile ya hali ya kutotumia mifumo badala yake kujikita katika kutumia sheria zaidi kuliko balagha.

Namna Polisi walivyotenda katika hali tete inaonesha ubora wa maandalizi ya jambo lenyewe. Kwa Tanzania, maofisa wanapitia mafunzo ya awali yanayoweka katika kusisitiza matumizi ya nguvu za kisheria, maadili, ukomo wa mamlaka na uwajibikaji.

Msingi huu huendelezwa kwa mafunzo kazini na kozi za kupandishwa vyeo, kwa kuhakikisha ujuzi na uzoefu zinahusiana na mabadiliko ya kijamii na kisiasa. Kazi ya polisi inazidi kutazamwa kama taaluma kuliko wito. Maofisa wanafunzwa katika ngazi mbalimbali za taaluma, kuanzia programu za astashahada na stashahada hadi vigezo vya shahada na stashahada za juu.

Maamuzi yote yanafanywa kwa kuzingatia miongozo ya kudumu na kanuni za operesheni, ambazo zimeweka taratibu katika kwenda kusimamia shughuli kama ilivyoonekana wakati wa uchaguzi. Suala la kusimamia utulivu katika jamii ni moja ya majukumu yanayoangaliwa sana kwa jeshi lolote la polisi. Matatizo yanayotokea baada ya upigaji kura huibuliwa katika mazingira yanayochagizwa na hisia za kisiasa, ambako uamuzi mbaya ungeweza kuzidisha hofu.

Mbinu za Polisi zinatoa kipaumbele kuzuia na kuchukua hatua za mapema za kuingilia kati. Doria za mara kwa mara, operesheni za kiintelejensia na kufuatilia maeneo yenye vihatarishi, zilitumika kutambua hatari kabla ya kusababisha ukosefu wa utulivu. Polisi jamii inaunda sehemu ya mkakati huu, kwa kuwafanya raia kuwa wabia katika kulinda amani kuliko kuwa walengwa wa usalama.

Yanapotokea maandamano, mikutano ya kisiasa au mikusanyiko ya kijamii, sheria inatoa fursa ya ulinzi. Majadiliano na waandaaji ni eneo la kuanzia, kuhakikisha matakwa ya kisheria yanatimizwa. Ni wakati pale masikilizano yanaposhindikana, au usalama wa jamii unapokuwa hatarini, ndipo polisi hutumia nguvu chini ya Sheria ya Jeshi la Polisi, Kanuni ya Adhabu na Sheria ya Makosa ya Jinai.

Hata hivyo, polisi wanatakiwa kuweka mizani katika matumizi ya nguvu na uhuru wa Katiba ikiwamo haki za kukusanyika na kujieleza. Uendeshaji wa polisi kisasa unasaidia kupunguza makali, na Jeshi la Polisi Tanzania limewekeza kikamilifu. Maofisa wa polisi wanapata mafunzo katika taasisi za ndani na nje ya nchi ya jinsi ya kudhibiti mikusanyiko, majadiliano na kuzuia migogoro.

Mbinu hizi zinaangazia ukweli kwamba jeshi pekee yake haliwezi kutatua mitanziko ya kisiasa. Lengo ni kuzuia matukio ya aina fulani kutoongezeka na kuwa vurugu kubwa zinazoweza kutishia utulivu wa taifa. Wakati wa kipindi baada ya uchaguzi, kujizuia na operesheni zilizoratibiwa kisasa zilisaidia kutuliza hali. ‘Kumulikwa’ kwa mwenendo wa polisi kumekuwa kukiongezeka katika kujikita kwenye kuheshimu haki za binadamu.

Nchini Tanzania, operesheni za polisi zinaongozwa na sheria za nchi pamoja na maridhio ya haki za binadamu kikanda na kimataifa. Mipango ya operesheni hasa zile zinazohusisha idadi kubwa ya askari, inaandaliwa kwa kuzingatia masuala hayo. SOMA: Amani iwe mtaji muhimu wa maendeleo 2026

Kukamata, kushikilia na kuhoji kunaongozwa na Sheria ya Makosa ya Jinai, Kanuni ya Adhabu na Sheria ya Ushahidi. Maofisa hupewa mafunzo ya mara kwa mara kuhusu haki za kikatiba na taratibu za kisheria. Mifumo ya uwajibikaji ni pamoja na mifumo ya ndani ya kinidhamu, madawati ya maadili na muundo wa kushughulikia malalamiko.

Jukwaa la kidijiti la e-Mrejesho limeongeza wigo wa kupata mrejesho, kuwawezesha raia na maofisa kuwasilisha malalamiko, maoni na mapendekezo moja ya kipengele muhimu cha uaminifu wa taasisi. Imani kama kipimo cha ufanisi Imani ya umma inasaidia kuleta ufanisi wa polisi kuliko rasilimali yoyote pekee.

Pale ambako imani imeshamiri, raia watakuwa tayari kuripoti uhalifu, kuchangia intelejensia na kutekeleza sheria. Polisi jamii imeimarisha uhusiano huu sehemu nyingi Tanzania. Ushirikiano na viongozi wa kijamii na mamlaka za serikali umeboresha mtitiriko wa taarifa na kuchangia kupungua kwa mienendo ya uhalifu mkubwa.

Na badala yake, hushawishi kubadili mtazamo wa jamii kama raia waione Polisi kama wabia au wapinzani. Kuendeleza mazuri haya kutahitaji uwekezaji endelevu. Bajeti ya mafunzo hasa kuhusu haki za binadamu, ya kuondoa migogoro na matumizi ya teknolojia inahitaji kuongezwa.

Polisi jamii itakuwa yenye manufaa makubwa ikihusianishwa na sera za kitaifa ili kuikinga kutoka katika duru za kisiasa. Maboresho katika vifaa, usafiri, mifumo ya mawasiliano na maslahi ya askari itasaidia kuimarisha mbinu za kiweledi. Raia pia wanapaswa kuwajibika. Ushiriki wa amani wa masuala ya kisiasa, kuheshimu utawala wa kisheria na kushirikiana na mamlaka ni mambo yasiyokwepeka, hasa wakati wa uchaguzi.

Ni ukweli usiopingika matukio ya Oktoba 29 na 30, 2025 yametoa mtihani kwa vyombo vya usalama nchini. Wakati maoni na kauli zikitofautiana, kipimo na muktadha wa hali unabainisha kuwa Jeshi la Polisi Tanzania lilitenda kazi zake kwa kufuata majukumu yake kisheria, yaliyochagizwa na mafunzo ya kiweledi na taratibu zilizowekwa za kulinda amani, utulivu na uimara wa taifa.

Hakuna mfumo wa polisi wa kuhakikisha amani inakuwapo ambao hauna upungufu, na usalama linabaki kuwa suala muhimu. Kwa kuangalia muktadha wa kidunia ambako migogoro ya baada ya uchaguzi imekuwa ikiendelea kusababisha vurugu kwa muda mrefu, kwa uzoefu wa Tanzania mfumo wake wa kulinda amani umezingatia kujizuia, sheria na ushirikiano.

Katika zama za siasa za kujitafutia umaarufu, mbinu kama hizo zinabaki kuwa zenye kuaminika kwa ajili ya kulinda amani ya nchi. Majukumu ni kulinda maisha, mali na usalama wa taifa kwa kusimamia taasisi za kisheria wakati wa uchaguzi, ambako hisia za kisiasa zinakuwa juu na upotoshaji unaweza kusambaa kwa haraka.

Katika wakati huo, kutokuwa na upande na utii kwa sheria inakuwa jambo gumu. Kuchukua hatua kwa polisi wakati huo wa matatizo kunasisitiza ile kanuni ya kwamba utulivu wa jamii si dhana dhahania, bali kitu cha lazima kwa raia kutimiza haki zao kwa usalama bila hofu. Matukio hayo pia yamewezesha kuweka wazi majukumu kati ya dola na jamii kuendeleza amani.

Wakati polisi wakiwa na jukumu la kusimamia sheria, raia, wadau wa siasa na vyama vya kiraia wote wana jukumu la kuweka mazingira safi ya usalama. Kauli za uchochezi, mikusanyiko isiyoruhusiwa kisheria na majaribio ya kuzidogosha taasisi za kiserikali, kunaongeza ugumu katika kusimamia utekelezaji wa sheria.

Nguvu ya kawaida iliyotumika wakati wa vurugu zile licha ya matukio kadhaa ya kipekee utaratibu wa ushirikiano na jamii na taasisi nyingine, ulionekana. Kwa kuangalia ulinganifu, uzoefu wa Tanzania umekuwa wa aina yake kikanda na kimataifa ambako migogoro ya uchaguzi mara nyingi imeibua kulipiza visasi, majeshi kuchukua uongozi na ukosefu wa utulivu kwa muda mrefu.

Katika nchi nyingi, makosa si tu yanaangukia katika mbinu za kipolisi, bali kukosekana kwa imani kati ya raia na vyombo vya usalama. Uwezo wa Jeshi la Polisi la Tanzania kujiendesha bila ya vurugu kuenea eneo kubwa kunaonesha thamani ya uwekezaji katika mafunzo, nidhamu ya kijeshi na kuheshimu mifumo ya kisheria. Hata hivyo, matukio haya yanapaswa kuwa somo si tu kama mtihani, bali fursa kwa mageuzi na kujifunza.

Kuimarisha polisi jamii, kuwa na uwazi katika operesheni na kuimarisha mawasiliano na jamii kutaweza kuzidisha imani. Wakati raia wakielewa somo kuhusu hatua za kiusalama, utii utaweza kuwa wa hiari zaidi kuliko kulazimishwa, hivyo kupunguza hatari ya mgogoro kuendelea.

Hatimaye, matukio ya Oktoba 29, yanatoa somo kuu: amani haiji kama ajali, na huwezi kuiwekea dhamana. Ni zao la taasisi ambazo zinafahamu majukumu yao, zinatimiza wajibu wake kwa busara na zinatambua kuwa uhalali unajengwa kwa kujizuia na kwa madaraka.

Na katika kuvuka kwenye matukio haya ya hofu baada ya uchaguzi bila ya kutumbukia zaidi kwenye machafuko, Jeshi la Polisi la Tanzania lilithibitisha jukumu lake ‘lisiloimbwa’ lakini muhimu, la usimamizi wa sheria kwa kuwa mstari wa mbele wakati taifa lilipokuwa kwenye mtihani ule.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Really insightful post — Your article is very clearly written, i enjoyed reading it, can i ask you a question? you can also checkout this newbies in seo. thank you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button