Namibia yapata rais mwanamke

NAMIBIA : HATIMAYE  wananchi wa Namibia wamemchagua rais wa kwanza mwanamke baada ya chama tawala cha SWAPO kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.

Tume ya Uchaguzi ya Namibia ECN, imemtangaza Makamu wa Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah, kushinda kwa zaidi ya asilimia 57 ya kura akifuatiwa na mgombea wa chama kikuu cha upinzani cha Patriots for Change IPC, Panduleni Itula aliyepata asilimia 25.5.

Hatahivyo, kambi ya upinzani imesema haitambui matokeo ya uchaguzi huo ambao wanadai ulikumbwa na udanganyifu mkubwa. SOMA: Namibia kutegemea kupata Rais mwanamke

Advertisement

Nandi-Ndaitwah mwenye miaka 72, anakuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo kupitia chama cha SWAPO kianchoongoza tangu  nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1990.