Nandy kushindana na Alade, Tiwa AEAUSA

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Faustina Mfinanga ‘Nandy’ ametajwa kuwania tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) katika kipengele cha ‘Best Female Artist’ akishindana na wasanii kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Simi, Ayra, Tems, Makhadzi, Tyla, Nandy, Aya Nakamuru na Niniola.

Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ anachuana na mastaa kutoka Nigeria katiika tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa Novemba mwaka huu.

AEAUSA wametoa orodha ya wasanii na vingengele watakavyowania katika tuzo hizo, ambapo katika kipengele cha ‘Artist of the Year’ Diamond atatoana jasho na mastaa kama Burna Boy, Davido, Yemi, Ayra, Asake, Rema, Wizkid, Adekunle na msanii kutoka Afrika Kusini, Tyla.

Mbali na kutajwa katika kipengele hicho, Diamond pia yupo kwenye kipengele cha ‘Best Male Artist’ akichuana na wasanii kama Davido, Harmonize, Burna Boy, Wizkid, Olamide, Rema, Kizz Daniel, Black sheriff na Fally Ipupa.

Habari Zifananazo

Back to top button