‘Navutiwa na dini ya kiislam’

MSANII wa filamu nchini, Jacqueline Wolper, amezua mjadala mpana mitandaoni baada ya kuweka wazi hisia zake kuhusu dini ya Kiislamu akieleza kuvutiwa kwake na imani hiyo. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Wolper amesema amekuwa akiguswa na baadhi ya vipengele vya dini ya Kiislamu hususan sauti za adhana, swala na kaswida ambazo humgusa kihisia na kumpa amani ya moyo.

“Napenda sana kusikia swala na kaswida za Kiislamu. Nasisimkwa na kufurahia. Kuna wakati hata nilitamani wanangu waijue dini hii pia, pamoja na ya kwao. Sijui nakosea? Sijui ni nini?” aliandika Wolper. SOMA: Nicole afunguka urafiki na Wolper

Wolper pia ameeleza kuwa mapenzi yake kwa imani hiyo si ya juu juu bali ni hisia za ndani zinazomfanya wakati mwingine kushindwa kuzuia machozi anaposikia dua au nyimbo za dini hiyo. Aidha, amewahimiza Waislamu kuendelea kusali bila kuchoka akisisitiza kuwa hata kutoka upande mwingine wa dini kuna watu wanaopenda na kuheshimu wanachokifanya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button