Mpira unaumiza jamani daah!

ZANZIBAR; MPIRA UNAUMIZA, lakini mpira pia unakera. Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa mwisho hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na JS Kabylie uliomalizika muda mfupi uliopita Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na Yanga kushinda mabao 3-0.

Ndiyo mpira unaumiza kwani licha ya ushindi huo mnono, Yanga imekwama kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya Al Ahly ya Misri na FAR Rabat ya Morocco kutoka 0-0 katika mchezo wao wa mwisho wa ligi hiyo mjini Cairo, Misri.

Timu zote zimemaliza michezo ya makundi, ambapo Al Ahly inaongoza ikiwa na pointi 10, FAR Rabat imeshika nafasi ya pili ikiwa na pointi tisa na Yanga nafasi ya tatu ikiwa na pointi nane, huku Kabylie ikiburuza mkia ikiwa na pointi tatu.

Kutokana na matokeo hayo timu mbili za juu zinatinga robo fainali, huku Yanga ikiungana na timu nyingine ya Tanzania,  Simba ya Dar es Salaam ambayo nayo imeshindwa kufuzu robo fainali baada ya kuburuza mkia kwenye kundi lake Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here …………………… http://www.giftpay7.vip

  2. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  3. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button