“Nawasihi kuzingatia sheria ya usalama barabarani”

MTANDAO: RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuzingatia sheria ya usalama barabarani na kuchukua tahadhari na umakini mkubwa katika juma la mwisho kuufunga mwaka 2023 lenye sikukuu mbili za Krismasi na Mwaka Mpya.

 

Rais Samia ametuma ujumbe huo kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii katika kuwatakiwa heri Watanzania katika kuadhimisha sikukuu za mwishoni mwa mwaka 2023.

Advertisement

“Katika sherehe hizi, baadhi yenu mnasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kujiunga na familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawasihi kuzingatia sheria ya usalama barabarani na kuchukua tahadhari na umakini mkubwa ili juma hili likawe lenye furaha,” ameandika Rais Samia.

Amesema, mkawe na muda mzuri na ndugu, jamaa na marafiki, na baadaye nyote mrejee mkiwa wazima wa afya kuendelea kufanya kazi ya kuliletea taifa letu maendeleo.

 

“Namuomba Mwenyezi Mungu ili sote tuweze kufikia siku hizi tukiwa wazima wa afya, kusherehekea kwa pamoja, kwa upendo, amani, furaha na usalama.” Salamu za Mkuu wa Nchi kwa Watanzania.

 

1 comments

Comments are closed.