Nchimbi: Tanzania imedhamiria kulinda afya, maisha ya watu
Makamu wa Rais Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema Tanzania imedhamiria kuhakikisha inalinda afya, maisha ya watu na mazingira kwa kutoa kipaumbele katika uimarishaji wa mfumo wa afya, kuwekeza katika utafiti wa kisayansi, na kuhimiza matumizi ya dawa kama yanavyokusudiwa kwa manufaa ya watanzania na dunia kwa ujumla.
Dk Nchimbi amesema hayo wakati akifungua Maadhimisho ya Kanda ya Afrika ya Wiki ya Kimataifa ya Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa, yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema hatua hizo ni katika kukabiliana na tishio linaloongezeka la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, ambapo pia ametoa wito kwa nchi za Afrika kujiunga katika mapambano hayo ya kimataifa kwa kuunga mkono juhudi za matumizi sahihi ya dawa hizo za kuokoa maisha, kwa kubadilishana ujuzi, kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha kwamba dawa za vimelea vya magonjwa zinabaki kuwa na nguvu kwa vizazi vijavyo.
SOMA: Dk Magembe: Matumizi holela ya dawa janga jipya
Halikadhalika, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa kupitia kubadilishana takwimu na uratibu wa utekelezaji wa sera katika mapambano dhidi usugu wa vimelea vya magonjwa.
Amesema ushirikiano huo ni muhimu kwa kuwa maambukizo hayazuiliwi na mipaka ya kijiografia.

Vilevile, Makamu wa Rais amesema uwekezaji katika uvumbuzi na utafiti ni muhimu kwa lengo la kuboresha zana mpya za uchunguzi, chanjo na matibabu mbadala ambayo yanaweza kupunguza utegemezi kwa dawa za asili za vimelea vya magonjwa na kuweza kudhibiti mabadiliko ya magonjwa yanayojitokeza kwa jamii moja moja.
Pia, Makamu wa Rais ametaja umuhimu wa utoaji elimu kwa umma na ushirikishwaji wa jamii ili kuwezesha wananchi kufuata ushauri wa huduma ya afya, kukamilisha dawa zilizoagizwa, kuepuka matumizi mabaya ya dawa za vimelea vya magonjwa na dawa zinginezo na kuzingatia viwango vya kuzuia na kudhibiti maambukizi.

Makamu wa Rais amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa, Tanzania ina dhamira ya kuongeza juhudi za kukabiliana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa kupitia mipango mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji ili kuwa sera na afua zinazozingatia ushahidi.

Vilevile, kuongeza hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi kote katika huduma za afya, shamba na mazingira ya jamii ili kupunguza kuenea kwa magonjwa sugu, kuimarisha matumizi sahihi ya dawa za vimelea vya magonjwa katika sekta ya afya ya binadamu na wanyama, kutekeleza mifumo thabiti ya udhibiti na uangalizi ili kuzuia matumizi mabaya ya dawa za kuua vimelea vya magonjwa, pamoja na kuendeleza utafiti, uvumbuzi, na suluhu mbadala ili kuwa na ufanisi wa dawa.
Maadhimisho hayo yanayofanyika Desemba 2 hadi 5, 2025 yanashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya Barani Afrika yakiwa na kauli mbiu, “Chukua hatua sasa: Ilinde leo, kuwa na kesho salama.”




Epuka kujiunga au kushiriki kwenye makundi ya mtandaoni yanayochochea vurugu. Ni kosa kwa mujibu wa sharia.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… Y You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good eaning opportunity.tab for more detail thank you……..
For details check ——-⫸ http://www.join.money63.com
I am making a good salary from home $7580-$9065/week , which is amazing, under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions, Definitely a try..
See This Link………………………………….. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
Epuka kujiunga au kushiriki kwenye makundi ya mtandaoni yanayochochea vurugu. Ni kosa kwa mujibu wa sharia..
Epuka kujiunga au kushiriki kwenye makundi ya mtandaoni yanayochochea vurugu. Ni kosa kwa mujibu wa sharia.
Epuka kujiunga au kushiriki kwenye makundi ya mtandaoni yanayochochea vurugu. Ni kosa kwa mujibu wa sharia.
Epuka kujiunga au kushiriki kwenye makundi ya mtandaoni yanayochochea vurugu. Ni kosa kwa mujibu wa sharia.