Ndumbaro asisitiza elimu zaidi kuhusu bima

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA), imetakiwa kuongeza juhudi za kuendelea kujenga ufahamu kwa wananchi ili kuleta mafanikio katika sekta hiyo.

Wito huo umetolewa na Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo,  Dk Damas Ndumbaro wakati wa ufunguzi wa taarifa ya utendaji wa soko la bima kwa mwaka 2022, Desemba 6 2023 jijini Dar es Salaam.

“Bado mitazamo ya watu na uelewa kwenye bima na bidhaa zake na umuhimu wake bado ni mdogo sana. Ukiuliza Watanzania wengi wanasema bima ni kwa ajili ya gari, na ni kwa sababu sheria inawalazimisha,” amesema Ndumbaro.

Advertisement

Dk Ndumbaro amesema kuna haja ya kuboresha mifumo ya huduma na bidhaa za bima kwa wateja kidijitali na kuhakikisha upatikanaji wa huduma hizo wanazipata kiurahisi kwa wakati.

Aidha amesistizia juu ya umuhimu wa bima ya afya, ambapo utaleta uwepo wa upatikanaji wa huduma za afya bila matabaka.

Naye  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Bima, CPA Moremi Marwa  amesema licha ya changamoto zilizopo katika sekta ya bima lakini wakazifanya kuwa fursa ili kuendelea kufanya vizuri zaidi.

” Maendeleo ya sekta ni mazuri ila changamoto tuzikubali ili kufika kule tunapotegemea kuendelea kufanya vizuri zaidi,” amesema Moremi.

Ametaja sababu zilizochangia ukuwaji wa soko la bima nchini ni kuwepo na ongezeko kubwa la taasisi zinazotoa huduma ya bima pamoja na ongezeko la wateja  inayoleta maendeleo chanya.

 

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *