BARAZA la Mitihani Nchini (NECTA) limefuta matokeo yote ya watahiniwa 2194 sawa na asilimia 0.16 ya watahiniwa milioni 1.35 waliofanya mitihani na kubainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022.
MATOKEO YA DARASA LA SABA ANGALIA HAPA>>>https://necta.go.tz/psle2022/psle.htm
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi amesema watahiniwa zaidi ya 1.07 milioni kati ya 1.34 milioni wenye matokeo sawa na asilimia 79.62 wamefaulu kwa kupata madaraja A na B na C.
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 2,194 wa mtihani wa mwisho wa darasa la saba sawa na asilimia 0.16 ya watahiniwa milioni 1.3 baada ya kubainika kufanya udanganyifu katika mitihani yao, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi amesema. pic.twitter.com/qigdFkgTRy
— HabariLeo (@HabariLeo) December 1, 2022
Amesema takwimu zinaonyesha upungufu wa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 165, 600 sawa na asilimia 18.24 ikilinganishwa na mwaka jana.
Aidha, baraza hilo limevifungia vituo vya mitihani 24 ambavyo vimethibitika kufanya undanganyifu katika mtihani huo hadi hapo baraza litakapojiridhisha ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa.
MATOKEO YA DARASA LA SABA ANGALIA HAPA>>>https://necta.go.tz/psle2022/psle.htm