ZANZIBAR; MSANII wa muziki wa bongo fleva kutokea Zanzibar Said Seif Ally maarufu Nedy Music amesema kuna haja sasa kwa shirikisho la sanaa visiwani humo kuandaa tamasha kubwa la wasanii ili waongeze umoja wao lakini pia wawape mbinu mbalimbali za kunufaika na soko la sanaa wanazofanya ili waendane na kasi ya kukuwa kwa teknolojia.
Nedy Music aliyeanza muziki kibiashara mwaka 2012 na sasa anatamba na wimbo wa ‘Nigee’ anasema alitamani kuanzisha tamasha lake kama baadhi ya makampuni na wasanii wa bara wanavyofanya lakini ameona ni vyema kwanza kukawa na tamasha moja kubwa litakalokuwa kila mwaka likihusisha wasanii wa sanaa zote.
“Napenda kuwa na tamasha langu la muziki kisha nikafanya maonesho sehemu mbalimbali za Zanzibar kama tamasha la fiesta, wasafi, mziki mnene, Nandy, Konde Gang na mengine mengi lakini kwanza kunahitajika hamasa na elimu ya uelewa wa sanaa mbalimbali ikiwemo muziki kwa Zanzibar ndipo matamasha mengine yafanyike,” alisema Nedy.
Nedy alisema kwamba anaimani wakati ukifika wahusika wasanaa Zanzibar watawakutanisha wasanii wa fani mbalimbali wa Zanzibar katika tamasha moja na kuwapa elimu ya namna ya kunufaika na sanaa zao maana teknolojia inazidi kukua lakini wasanii wengi hawajui namna ya kuitumia ili kwenda nayo sambamba.
Comments are closed.