NEMC yaadhimisha siku ya usafi duniani hospitali Mwananyamala

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), katika kuadhimisha Siku ya Usafi Duniani loe Septemba 20, 2025 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira wakiwemo DEPO, limefanya usafi Hospitali ya Mwananyamala na maeneo mengine nchi nzima ambapo Kanda 13 zikitoa huduma za Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira.

SOMA: NEMC yaja na usafi kampeni 2025

Zoezi hilo limehusisha watumishi wa NEMC, wawakilishi kutoka DEPO pamoja na baadhi ya wananchi wa maeneo ya jirani, ambapo usafi mkubwa umefanyika katika mazingira ya hospitali hiyo, ikiwa ni pamoja na kuondoa taka, kufagia, na kusafisha mitaro ya maji taka.

Akizungumza katika zoezi hilo, Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kaskazini, Glory Kombe amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuwa na mazingira safi, salama na endelevu kwa afya na maendeleo ya Taifa.

“Siku hii si ya kusherehekea tu, bali ni ya kutafakari na kuchukua hatua. Mazingira safi ni msingi wa afya bora, ukiangalia taka zilizookotwa hapa nyingi ni za majumbani, kuna mifuko ya plastiki, chupa, mabaki ya vyakula ambazo zingetakiwa kutenganishwa kutokea nyumbani. Tuna wajibu wa pamoja kuhakikisha tunatunza mazingira yetu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa DEPO,  Humphrey Milinga ameeleza kuwa ushirikiano kati ya mashirika ya mazingira na Taasisi za afya ni hatua muhimu katika kuhakikisha jamii inapata huduma katika mazingira rafiki na salama.

“Tumeona ni vyema kufanya usafi hospitalini kwani ni maeneo ya kuhudumia afya, na mazingira yake yanapokuwa safi, yanasaidia kuzuia maambukizi ya magonjwa,” ameongeza.

Katika maadhimisho hayo, kanda mbalimbali za NEMC pia zimetekeleza shughuli za usafi katika maeneo yao husika, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya usafi inayolenga kuhamasisha ushiriki wa jamii nzima katika kulinda mazingira.

Siku ya Usafi Duniani huadhimishwa duniani kote Septemba 20 kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha watu kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira, kuondoa taka, na kuelimisha jamii juu ya athari za uchafuzi wa mazingira.

NEMC imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi yenye mazingira safi na salama kwa wote.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google paid $220 an hour on the internet. My close relative has been without labor for nine months and the earlier month her compensation check was 25k by working at home for 10 hours a day….. Everybody must try this job now by just use this link

    COPY THIS→→→→ http://Www.Work99.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button