DAR ES SALAAM; Brown-Forman Corporation na Kampuni ya Coca-Cola wameingiza mtaani kitu kipya ambacho ni kileo kilicho tayari kwa kunywewa (ARTD) .
“Tunafurahi kuleta Jack Daniel’s na Coca-Cola kwenye soko la Afrika na kuwapa watumiaji njia mpya na ya kusisimua ya kufurahia mchanganyiko wa chapa zetu mbili za kipekee,” amesema Peter Orfanidis, Meneja wa Kanda wa Brown-Forman na kuongeza:
“Tunapoendelea kusikiliza wateja kupitia bidhaa zetu mpya na kupanua upatikanaji wa Jack Daniel’s na Coca-Cola duniani kote, tunafurahi kuanzisha kinywaji hiki kilichohamasishwa na moja ya kokteili maarufu zaidi duniani.”
Amesema kinywaji hicho ambacho ni mchanganyiko wa Jack Daniel’s na Coca-Cola, ni kionjo kikamilifu cha kufurahia wakati mzuri na marafiki.
Soma pia: ‘Beetroot’ sasa kutengenezwa mvinyo
“Bidhaa hii mpya inaonesha kujitolea kwetu kuleta uzoefu bora wa ladha kwa watumiaji katika muundo rahisi wa kuwa tayari kunyweka,” amesema Natasha Chetty, Mkurugenzi Mtendaji wa Bidhaa mpya katika kampouni ya Coca-Cola Afrika.
Amesema kuingizwa mtaani kwa kinywaji hicho kunaonesha dhamira ya dhati ya kampuni ya Coca-Cola ya kuwafanya wateja wake kuwa na furaha muda wote kwa kuwa na bunifu mbalimbali za kuwaburudisha.
Imeelekezwa kuwa baada ya kuzinduliwa kwa mafanikio katika masoko zaidi ya 25 duniani kote yakiwemo ya Marekani, Mexico, na Japan kinywaji cha Jack Daniel’s na Coca-Cola ARTD sasa kimefika Dar es salaam katika bara la Afrika.
Uzinduzi ulijumuisha aina mbili za vinywaji yaani, Jack Daniel’s na Coca-Cola ya asili, na toleo la Coca-Cola Zero Sugar, ili kukidhi mapendeleo tofauti ya watumiaji.
Msemaji wa Coca-Cola akizungumza katika uzinduzi alisema kampuni yake inaelewa jukumu lake muhimu katika kukuza kunywa kwa uwajibikaji miongoni mwa wale waliofikisha umri wa kisheria wa kunywa, na itafuata sera yake ya uuzaji wa pombe kwa uwajibikaji inayoongoza katika sekta hiyo.