Ni Taifa Stars ya viwango

DAR ES SALAA; BAO la dakika ya 89 lililofungwa na beki wa kulia Shomary Kapombe limeipa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ pointi tatu muhimu kwa kuifunga Mauritania bao 1-0.

Mchezo huo wa Kundi B katika fainali za CHAN umemalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.



