Ni ubabe tena Euro 2024 leo

BAADA ya Ujerumani na Hispania kukata tiketi ya hatua ya 16 michuano ya Euro 2024 inayoendelea Ujerumani, leo UHOLANZI au Ufaransa mojawapo ina nafasi kusonga mbele iwapo itashinda mchezo kati yao.

Timu hizo zina pointi 3 kila moja baada kushinda michezo ya kwanza hivyo itakayoibuka mbabe katika mechi ya leo ya kundi D kwenye uwanja wa Red Bull uliopo jiji la Leipzig itatinga 16 bora.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Poland itaivaa Austria kwenye uwanja wa Olympia uliopo jiji la Berling, zote hazina pointi baada kupoteza mechi za awali.

Slovakia na Ukraine zitaoneshana kazi katika uwanja wa Merkur Spiel uliopo jiji la Düsseldorf ukiwa mchezo wa kundi E.

Habari Zifananazo

Back to top button