NIGERIA: Hatma ya Burkina Faso, Mali na Niger kujulikana kesho

NIGERIA : HATUA ya mataifa ya Burkina Faso, Mali na Niger ya kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) itaidhinishwa rasmi hapo kesho baada ya mwaka mmoja wa mivutano ya kisiasa.

Mnamo Januari 29, 2024, nchi hizo tatu zinazoongozwa na serikali za kijeshi ziliarifu rasmi ECOWAS juu ya uamuzi wa kujiondoa kwao, lakini katiba ya jumuiya hiyo inaeleza kuwa uamuzi kama huo huidhinishwa rasmi baada ya mwaka mmoja.

Burkina Faso, Mali na Niger, ambazo sasa zimeungana katika shirikisho linalofahamika kama  Muungano wa Nchi za Sahel (AES), zinaishutumu ECOWAS kwa kuziwekea vikwazo walivyovitaja kuwa vya  visivyo halali baada ya mapinduzi yaliyowaweka madarakani watawala wa kijeshi.

SOMA:  Niger, Burkina Faso, Niger zachukua sura mpya Ecowas

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button