Nyamapori bila kibali yamtupa jela miaka 10

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 10 jela, Kedo Malikani, mkazi wa Kijiji cha TuombeMungu wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande vinne vya nyama ya mnyamapori kinyume na sheria ya nchi.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, Jovith Kato alisema ushahidi uliotolewa na Jamhuri mbele ya mahakama hiyo umeonyesha alitenda kosa hilo.

Alisema anatoa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojiusisha na biashara haramu ya kuuza nyama za pori posikuwa na kibali kinachotolewa na mamlaka inayousika na maliasili.

Hakimu Kato alisema mshitakiwa ametiwa hatiani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi baada ya kupatikana na vipande vinne vya nyama ya porini pamoja na risasi tatu za bunduki aina ya gobore katika hifadhi ya Msitu wilayani Kaliua.

Akitoa maelezo ya awali katika shauri hilo namba 6 la mwaka 2022, Wakili wa Serikali, Alice Thomas aliiambia mahakama hiyo kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo kwenye moja ya hifadhi za Kaliua Januari 28, mwaka huu ambapo alikutwa na vipande hivyo vya nyama ya pori.

Alisema vipande hivyo alivyokutwa navyo mshitakiwa vyote vina thamani ya zaidi ya Sh milioni 2.

3.

Aidha, mshitakiwa huyo kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo aliomba Mahakama imwachie huru ili akaendelee na shughuli zake.

Habari Zifananazo

Back to top button