Nyota Yanga wamkosha Pedro

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, amekoshwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake akisema wataendelea kupambana kushinda na kulinda heshima ya rangi zake.
Kauli hiyo inakuja baada ya Yanga kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Amesema ushindi huo umetokana na dhamira ya pamoja ya kikosi kizima kuanzia benchi la ufundi hadi kwa wachezaji waliokuwa uwanjani, akisisitiza kuwa Yanga itaendelea kupambana kushinda na kulinda heshima ya rangi zake.

“Ni ushindi mkubwa uliopatikana kwa kujituma na kujitoa kwa hali ya juu kutoka kwa kila mmoja. Tunataka kuendelea kushinda na kuheshimu rangi za Yanga,” amesema.
Yanga ilitawala mchezo huo kwa kiwango kikubwa, ikionesha soka la kasi, pasi za uhakika na umakini mkubwa katika umaliziaji, hali iliyoifanya Mashujaa kushindwa kuhimili presha tangu dakika za mwanzo hadi mwisho wa mchezo.
Ushindi huo uliipandisha Yanga kutoka nafasi ya pili hadi katika uongozi wa ligi kwa kufikisha pointi 19.




Hongera yanga,mkafanye vizuri pia kimataifa.
l Get paid over $110 per hour working from home. l never thought I’d be able to do it but my buddy makes over $21269 a month doing this and she convinced me to try. The possibility with this is endless….
This is what I do………………………………….. https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
This is what I do………………………………….. https://Www.Payathome9.Com