Ofisi 11 Takukuru kujengwa mwaka wa fedha 2025/26

GEITA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imepanga kujenga majengo 11 kwa mwaka wa fedha 2025/26 kati yake ofisi moja ya mkoa sambamba na ofisi 10 za wilaya nchi nzima.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Crispin Chalamila ametoa taarifa hiyo katika hafla ya uzinduzi wa jengo la ofisi za Takukuru wilayani Nyang’hwale mkoani Geita.

Crispin amesema mpaka sasa kuna uhitaji wa jumla ya ofisi 64 ambazo bado hazijafikiwa kujengewa ofisi katika mikoa minne, wilaya 55 na vituo maalum vitano.

“Takukuru imeweka mkakati endelevu wa kutenga bajeti ya kujenga bajeti zake kila mwaka, mpaka sasa Takukuru ina ofisi 145 katika mikoa ya kitakukuru 28, wilaya 111 na vituo malum sita.

“Kati ya ofisi hizo 145, majengo ya Takukuru yanayomiikiwa na mikoa ni 70 peee katika mikoa 23 wilaya 46 na kituo maalum kimoja”, amesema Crispin.

Amesema dhamira ya Takukuru ni kujenga mazingira bora ya watumishi kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi na kuwajibika kikamirifu kwa mjibu wa malengo na majukumu ya taasisi hiyo nchini.

“Hatuna budi kuhakikisha kuwa tunatekeleza wajibu yenye dhamira ya kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maono ya serikali ya kujenga Tanzania isiyo na changamoto za rushwa”, amesema Crispin.

Mkurugenzi wa Miliki TAKUKURU, Emmanuel Kiyabo amesema mradi wa jingo la ofisi za Takukuru Nyang’hwale umetekelezwa kwa bajeti yam waka wa fedha 2024/25 kwa bajeti ya awali ya Sh milioni 385.

Amesema mradi jingo la ofisi ulianza kutekelezwa Februari 17, 2025 mpaka kukamilika limegharimu kiasi cha Sh milioni 386 ambapo kuna ongezeko la takribani 600,000 kutoka kiwango cha bajeti ya awali.

“Sisi watumishi wa Takukuru, tunaahidi kuyatunza majengo haya huku tukiendelea kuchapa kazi kwa uaminifu, kwa weledi, kwa uzalendo na kwa umahili mkubwa katika majukumu yetu”, amesema.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Geita, James Ruge amewakikishia wakazi wa Geita kuwa majukumu ya Takukuru yanaendelea kutekelezwa kwa taratibu za uchunguzi, uelimishaji umma, kuzuia rushwa na huduma za sheria.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    THIS→→→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button