Pacome aitwa Ivory Coast

KIUNGO wa Young Africans, Pacome Zouzoua ameitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu yake ya taifa.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast (IFF) Pacome anachukua nafasi ya Ibrahim Sangare anayechezea Nottingham Forest ya Uingereza.

‘The Elephants watashiriki michezo miwili ya marafiki dhidi ya Uruguay na Benin mnamo Machi 23 mwaka huu.

Advertisement

Hata hivyo haijathibitishwa kama mchezaji huyo atashiriki michezo hiyo kwani aliumia wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC.

Pacome mwenye mabao 7 Ligi Kuu amekuwa katika kiwango bora huku akishika nafasi ya pili ya wafungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na mabao manne.

Pacome Zouzoua kwa mara ya kwanza alijumuishwa kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 53 kilichoandaliwa kwa ajili ya AFCON 2023 lakini meneja wa zamani wa Ivory Coast, Jean-Louis Gasset alimtoa kwenye michuano hiyo.