Papa Francis kuzikwa jumamosi

VATICAN : MAZISHI ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis yamepangwa kufanyika siku ya Jumamosi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Bikira Maria Mkuu.

Vatican imetangaza kuwa waumini wataanza kuuaga mwili wa Papa Francis siku ya Jumatano katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter, siku chache baada ya papa huyo maarufu kufariki akiwa na umri wa miaka 88.

Makadinali wanakutana mjini Vatican kupanga maelekezo maalum kwa ajili ya mazishi ya Papa Francis.SOMA: Papa Francis afariki Dunia akiwa na miaka 88

 

 

Argentina, alikozaliwa Papa Francis, imetangaza wiki ya maombolezo ya kitaifa huku India ikianza siku tatu za maombolezo ya kitaifa hii leo.

Wakuu wa nchi pamoja na wafalme wanatarajiwa kuhudhuria mazishi ya Papa Francis , katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter, huku Rais wa Marekani Donald Trump akiwa wa kwanza kutangaza kuwa atahudhuria

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I’m getting 88 D0llars consistently to deal with net. Q I’ve never accepted like it tends to be reachable anyway one of my most noteworthy buddy got D0llars 27,000 D0llars in three weeks working this basic task and she impacted me to avail…
    Take A Look Here….> http://Www.HighProfit1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button