PICHA: Waziri Mkuu ashiriki Swala ya Eid

DAR ES SALAAM – Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 17, 2024 ameswali swala ya Idd El-Adh’haa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA, Kinondoni Dar es Salaam.

Baada ya Swala, Majaliwa aliongoza hafla ya Baraza la Kitaifa lililofanyika katika msikiti huo.

Baadhi ya Viongozi wengine walioshiriki swala hiyo pamoja na baraza la Idd ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa, Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila

 

Habari Zifananazo

Back to top button