Pinda aonya wasambazaji mbolea

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri kwa Rais katika masuala ya Kilimo na Chakula, Mizengo Pinda amewaonya viongozi na kampuni zilizopewa dhamana ya kusimamia na kusambaza mbolea za rukuzu kwa wakulima kuacha matumizi mabaya ya madaraka waliyopewa kusimamia zoezi hilo.

Akizungumza na wadau wa kilimo katika Wiki ya Mwanakatavi inayoendelea mkoani Katavi, Pinda amesema ili kufikia asilimia 10 ya sekta ya kilimo kuchangia pato la taifa ifikapo mwaka 2030 matumizi ya mbolea, mbegu bora na uhifadhi bora wa mazao lazima uzingatiwe.

Aidha amesema kuwa hivi sasa kwenye sekta ya kilimo matumizi ya mbolea yako chini na hii inachangiwa na baadhi ya wasimamizi waliopewa dhamana na serikali ya kusimamia utoaji wa mbolea kwa wakulima kutumia madaraka yao vibaya kuhujumu usambazaji wa mbolea kwa wakulima.

“Matumizi mabaya ya madaraka kwenye usambazaji wa mbolea kwa wakulima ni hali ya wasimamizi waliopewa dhamana na serikali kuwadanganya wakulima kuwa mbolea hazipo kwa lengo la kuzipeleka mahali pengine kwa ajili ya watu fulani na kusababisha kero kwa wakulima kushinda asubuhi hadi jioni wakitafuta mbolea bila mafanikio yoyote.”amefafanua Pinda.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akitoa hali ya maandalizi ya kilimo kwa msimu ujao wa kilimo wa 2023/2024 kwenye amesema kuwa umefika wakati kwa taasisi zinazosimamia matumizi bora ya mbegu kuongeza usimamizi ili kudhibiti na kutokomeza tabia hiyo ambayo ni chanzo cha uzalishaji mbaya wa mazao.

“Kuna baadhi ya watu wanatabia ya kuchukua mbegu za kawaida na kuzipaka rangi kisha kuzifunga kwenye mifuko vizuri na kuwauzia wakulima kumbe ni mbegu feki”amesema Mrindoko

Raymond Kamtoni ambaye ni miongoni mwa wadua wa kilimo walioshiriki amesema kuwa ili kufikia asilimia 10 ya sekta ya kilimo kuchangia pato la Taifa ifikapo mwaka 2030 serikali inapaswa kudhibiti mbolea zisizo na ubora pamoja na viuatilifu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MeghanMarkle
MeghanMarkle
1 month ago

Making extra salary every month from house more than $15,000 just by doing simple copy and paste like online job. I have received $18,000 from this easy home job. Everybody can now makes extra cash online easily.
.
.
Detail Here———————————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

Angila
Angila
1 month ago

Start your home business right now. Spend more time with your family and earn. Start bringing 99Dollars per hr just on a computer.(Qz) Very easy way to make your life happy and earning continuously…
.
.
.
This is where i started…>> http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x