Polisi waanza msako bajaji zinazohusika na uhalifu Morogoro

JESHI la Polisi mkoani Morogoro limefanya misako inayolenga kudhibiti mifumo inayozalisha uhalifu na wahalifu na kufanikisha kukamata pikipiki za magurudumu matatu ( Bajaji ) 31 kutokana na makosa ya usalama barabarabani vikiwemo vitendo vya udhalilishaji kwa abiria .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo , Alex Mkama amesema hayo machi 22, 2023 wakati akitoa taarifa kuhusiana na misako inayofanyika inayolenga kukabiliana na uhalifu na wahalifu ndani ya mkoa huo.

Mkama amesema Bajaji hizozinahusishwa na makosa mbalimbali yakiwemo kuambatana na wapigadebe wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo udhalilishaji (Vibeji).

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo ametaja makosa mengine yanayohusishwa ni kubeba abiria kupita uwezo wake , madereva kutokuwa na leseni na kukutwa na namba za usajili.

Mkama amesema katika msako huo unaendelea na pia mali kadhaa zimeokolewa na kupatikana ambazo ni Pikipiki tatu aina ya Teves yenye usajili MC .441 CQE, MC .841 DAR aina ya Boxer na MC 638 DDS aina ya Haojue , tv aina ya Mobiso na flash yake .

Mwisho.

Habari Zifananazo

Back to top button