JESHI la Polisi nchini limeteketeza silaha haramu 6,208 ambazo zilikusanywa wakati wa kampeni maalum ya wananchi kusalimisha silaha hizo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuongeza nguvu kudhibiti uingizaji silaha haramu ili kusaidia kupunguza matukio ya uvunjifu wa amani yanayo chochewa na ongezeko la silaha haramu nchini.
Akizungumza katika zoezi la uteketezaji silaha haramu katika viwanja vya Shabaha vya Jeshi la wananchi nchini(JWTZ), Sagini amesema waalifu wamekuwa wakitumia silaha hizo kwa kufanya vitendo viovu.
Amelitaka Jeshi la Polisi nchini kufatilia kwa ukaribu mikoa ambayo zinapatika Silaha hizo kwa wingi ili kubaini zinakotokea na kuziba mianya ya uingizaji silaha hizo.
Kamishna wa Jeshi la Polisi, Laberatatus Sabas, amesema kuwa jumla silaha 6208 zilizo salimishwa tangu kuanzishwa kwa kampeni maalumu ya kusalimishwa zimeteketezwa.
Uteketezaji wa silaha haramu ni takwa la kisheria katika Umoja wa Kanda ya Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya.
Jeshi la Polisi limesema kuwa litaendelea kuteketeza silaha haramu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ili waweze kutokomeza kabisa silaha haramu katika Jamii.