Precision kuboresha huduma zao

SHIRIKA la ndege la Precision limebainisha kuwa litaendelea kuboresha huduma zake hali itakayosaidia kukuza sekta ya usafirishaji nchini na hatimaye kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Patrick Mwanri amesema hayo leo wakati Shirika

hilo lilipowasafirisha kwa ndege abiria waliotakiwa kusafiri kwa basi kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Dodoma ikiwa ni katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Advertisement

Kwa upande wao baadhi ya abiria akiwemo Peter Joseph pamoja na Flora Mtawa wamelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kutoa huduma bora za usafirishaji huku wakibainisha umuhimu wa kuwa na machaguzi mengi pindi wanahitaji kusafiri.