Prof Mkenda: Wahitimu katekelezeni mageuzi ya elimu

DAR ES SALAAM: Serikali inawatarajia wahitimu katika mafunzo ya elimu kuwa mabalozi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema hayo alipozungumza kwenye mahafali ya 31 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).

“Katika kipindi hiki, tunawategemea sana kwenda kutusaidia kutekeleza mageuzi ambayo yameanishwa katika Sera mpya ya Elimu, pamoja na jukumu la kufundisha mtaenda kusimamia mabadiliko ya elimu nchini,” amesema.

buy solosec online https://sparkhealthmd.com/wp-content/uploads/2023/10/jpg/solosec.html no prescription pharmacy

Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dk Siston Masanja amesema serikali inawekeza katika mafunzo hayo ili kuwajengea walimu umahiri na uwajibikaji kwa maendeleo ya nchi.

“Wahitimu ni nguzo muhimu ya taifa, mnapaswa kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya ujenzi, usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji, kuzingatia usalama wa watoto pamoja na miongozo mbalimbali,” amesema.

Jumla ya Wahitimu 916 wametunukiwa stashahada, 702 ni wa kozi ya Stashaha ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu, 214 Stashahada ya Udhibiti Ubora wa Shule na wahitimu watatu wametunukiwa Astashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu.

buy inderal online https://sparkhealthmd.com/wp-content/uploads/2023/10/jpg/inderal.html no prescription pharmacy

Habari Zifananazo

Back to top button