Profesa Mkenda: Mabadiliko makubwa kwenye elimu yaja

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mabadiliko makubwa kwenye elimu yanakuja.

Alisema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha ‘Continuity with The Roadmap to Success for President Samia Suluhu Hassan’.

Alisema Rais Samia alitaka Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilitungwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Advertisement

“Sera iliyopo haijatekelezwa ambayo ilifanyiwa mapitio, elimu ya msingi mpaka darasa la sita, sekondari miaka minne ili mwanafunzi akae shuleni miaka 10,” alisema na kuongeza:

“Mabadiliko kwenye elimu yanakuja na yajayo yanafurahisha, tutapitisha kwenye Baraza la Mawaziri ili tupate kibali.”

Pia alisema kuwa watoto hujaza vitu vingi hali inayofanya hata kutoelewa lugha ya Kiingereza.