PSG yataka uhakika kumsajili Marcus Rashford

Fowadi wa Manchester United, Marcus Rashford.

TETESI za usajili zinasema Paris Saint-Germain itafikiria uhamisho wa fowadi wa Manchester United, Marcus Rashford na inaweza kuimarisha ufuatiliaji wapo itapokea hamasa kwamba nyota huyo yupo tayari kujiunga nayo. (Talksport)

Manchester City imeshindwa katika hatua ya hivi karibuni kuteka mpango wa uhamisho wa Michael Olise, 22, kutoka Crystal Palace kwenda Bayern Munich. (Football Insider)

Chelsea ina nia kumsajili beki wa Nottingham Forest mbrazil Murillo, 21, ambaye Forest imemweka katika thamani ya pauni mil 70 na inaweza kutoa ofa ya beki wa kati Trevoh Chalobah, 24, kama sehemu ya dili. (Guardian)

Advertisement

Aston Villa imekataa ombi la Tottenham la pauni mil 20 kumsajili kiungo Jacob Ramsey, 23, ikiwa ni dili linalojumuisha kiungo wa Argentina, Giovani lo Celso, 28, kuhamia upande mwingine. (Times)