PURA yaweka msisitizo elimu miradi kwa wananchi

MTWARA: Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeelekeza nguvu zake katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu miradi inayotarajiwa kutekelezwa kwa lengo la kuifanya kuwa na ufanisi kwa wazawa na taifa kwa ujumla.
Mamlaka hiyo imetoa msisitizo huo Oktoba 15, 2025 katika Kijiji cha Ruvula, mkoani Mtwara, wakati wa zoezi la utoaji wa elimu ya mradi wa uchimbaji wa visima vitatu vya gesi asilia unaotarajiwa kutekelezwa katika Kitalu cha Mnazi Bay kilichopo mkoani humo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mjiolojia Mwandamizi kutoka PURA, Ebeneza Mollel amesema kuwa, pamoja na kudhibiti shughuli za kitalaamu, PURA pia inahakikisha wananchi wanajengewa uelewa wa miradi kabla ya kuanza utekelezaji.
“Sisi kama Mamlaka tunahakikisha kuwa, jamii zinazoishi au zinazozunguka maeneo ambayo miradi ya mkondo wa juu wa petroli inatekelezwa, zinashirikishwa kikamilifu katika miradi hiyo na kujengewa uelewa wa kina kuhusiana na mradi,” alisema Mollel.
SOMA: Mamlaka Tanzania, Algeria zajadili kuinua sekta ya petroli, gesi asilia
Sambamba na hilo, mjiolijia huyo amebainisha kuwa Mamlaka hiyo inafuatilia kwa karibu hatua zote za utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa visima vya gesi asilia na kuwakumbusha watekelezaji wa mradi umuhimu wa utoaji wa uelewa wa mradi kwa wananchi.
Zoezi la utoaji wa uelewa wa mradi wa uchimbaji wa visima vya gesi asilia katika Kitalu cha Mnazi Bay linafanywa katika vijiji vitatu ambavyo ni Ruvula, Msimbati na Mtandi vilivyopo katika Kata ya Msimbati, Mtwara.
Mradi huo unaohusisha uchimbaji wa visima viwili vya uzalishaji na kisima kimoja cha utafiti unatarajiwa kugharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni 80.2 unatekelezwa na Kampuni ya Maurel et Prom Tanzania kwa kushirikiana na TPDC.
Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza Desemba 2025 ambapo utawezesha, pamoja na mambo mengine, ongezeko la uzalishaji wa gesi asilia kwa wastani wa futi za ujazo milioni 30 kwa siku.
Ongezeko hilo litasaidia upatikanaji wa gesi asilia kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, kwenye viwanda, majumbani na kwenye vyombo vya usafiri (magari na bajaji).
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com