Raha zaidi kuleee Robo Fainali

DAR ES SALAAM; TIMU ya Taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imemaliza mechi zake za makundi fainali za CHAN 2024 kwa kutoka 0-0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati mchezo uliomalizika usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo Taifa Stars imemaliza Kundi B ikiongoza ikiwa na pointi 10, baada ya kushinda michezo mitatu ya mwanzo.
Madagascar imeshika nafasi ya pili ikiungana na Stars kucheza robo fainali baada ya kuifunga Burkina Faso mabao 2-1, hivyo kufikisha pointi 7 sawa na Mauritania isipokuwa Madagascar ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button