Maduro aanza kudhibiti usalama

VENEZUELA : RAIS wa Venezuela, Nicolas Maduro, ametia saini amri inayompa mamlaka ya ziada ya kudhibiti hali ya usalama nchini humo. Makamu wa Rais, Delcy Rodriguez, amesema amri hiyo inamruhusu Maduro kudhibiti hali ya usalama kwa muda wa siku 90, na uwezekano wa kuongezwa kulingana na katiba ya nchi.

Hatua hiyo inajiri wakati Marekani imepeleka manowari za kivita katika eneo la Caribbean, hatua ambayo serikali ya Maduro inasema ni njama ya kumuangusha madarakani, huku Washington ikidai kuwa ni sehemu ya vita dhidi ya dawa za kulevya. SOMA: Uteuzi wa Rais Maduro hali ni tete

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button