Rais Museveni, Kikwete wakutana Uganda

RAIS wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika (AU) kwa Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu.

Mazungumzo hayo yamefanyika Jumanne, Aprili 7, 2027, katika Ikulu ndogo ya Nakasero jijini Kampala, Uganda. Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili hali ya kisiasa na kiusalama nchini Sudan Kusini, wakisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya amani na maridhiano miongoni mwa pande zinazohusika ili kurejesha utulivu wa kudumu.

Museveni amemweleza  Kikwete kuwa Uganda itaendelea kuunga mkono juhudi zote za kuleta amani nchini Sudan Kusini. Amebainisha kuwa utulivu wa nchi hiyo, hususan katika eneo la Equatoria lenye idadi kubwa ya raia wa Uganda, ni muhimu kwa usalama wa kikanda na ustawi wa kiuchumi.

Kwa upande wake, Dk. Kikwete ameeleza dhamira ya Umoja wa Afrika kuimarisha juhudi za upatanishi na utatuzi wa migogoro katika ukanda huo. Hivi karibuni, Kikwete ameteuliwa kuwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika kwa Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu, jukumu linalolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda pamoja na kusukuma mbele ajenda ya amani katika eneo hilo linalokabiliwa na changamoto za kisiasa na kiusalama.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

    2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity……….
      .
      This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  2. My pay at least $300/day.My co-worker says me!I’m really amazed because you really help people to have ideas how to earn money. Thank you for your ideas and I hope that you’ll achieve more and receive more blessings. I admire your Website I hope you will notice me & I hope I can also win your paypal giveaway.

    go to this link…………… w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button