Rais Mwinyi aipongeza zabesa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amekipongeza Chama cha Mchezo wa Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA), kwa utaratibu wa kuwaunganisha wananchi kufanya mazoezi.
Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na uongozi wa chama hicho ukiongozwa na Mwenyekiti wake Said Suleiman Said.
Amesema hamasa inayotolewa katika ufanyajaji Mazoezi ni njia sahihi katika kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni hamasa yenye tija, pia amewaasa kuendelea kuwashawishi wananchi zaidi waendelee kujiunga katika vikundi hivyo walio katika vikundi wasitoke.
Dk.Mwinyi amewaunga mkono na kuwapongeza kwa utaratibu wa kufanya usafi katika kisiwa cha Changuu na ameunga mkono wazo la Siku ya Jumamosi kuwa siku ya usafi na ameshauri ili vikundi viwe kimaendeleo zaidi katika Uanzishwaji wa shughuli za uzalishaji mali kwa maana inakuwa rahisi kwa Serikali kuwasaidia wakiwa katika vikundi .
Amewataka ZABESA kushirikiana na sekta binafsi hasa makampuni ya simu na benki kufanikisha matamasha yao kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu ufanyajaji Mazoezi na usafi wa Mazingira .
Dk.Mwinyi amewaahidi kushirikiana nao kutafuta waatalamu wa Mazoezi ambao watakuwa watajitolea kufundisha vikundi mbalimbali aina za ufanyaji wa Mazoezi.
Mwenyekiti wa chama hicho ndugu Said amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kutimiza miaka miwili ya Uongozi wake kwa Maendeleo anayowaletea Wazanzibari , pia kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar.