Rais Mwinyi atangaza mwelekeo mpya SMZ

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi Baraza la 11 la Wawakilishi Zanzibar na kutoa mwelekeo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kipindi cha pili cha Awamu ya Nane, akisisitiza azma ya Serikali kuendeleza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa msingi wa amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Chukwani, Unguja, Rais Mwinyi alisema Serikali itaendelea kutekeleza Ilani ya CCM 2025–2030, pamoja na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza cha uongozi wake.

Alisema Serikali itaendeleza mageuzi ya kiuchumi kupitia uimarishaji wa sekta za uzalishaji, uwekezaji na teknolojia za kisasa, ikiwa na lengo la kuongeza ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 7 hadi 10 kwa mwaka, kudhibiti mfumko wa bei chini ya asilimia 5 na kuzalisha ajira mpya 350,000 kufikia mwaka 2030.

Rais Mwinyi alitaja miradi mikubwa inayotarajiwa kutekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa bandari jumuishi ya Mangapwani, bandari za abiria Mpigaduri, Kizimkazi, Shumba na Wete, pamoja na boti mbili za kisasa zitakazohudumia safari kati ya Unguja, Pemba, Tanga na Dar es Salaam.

Katika sekta ya afya, Serikali itajenga hospitali nne za mikoa, kuendeleza ujenzi wa Hospitali ya Saratani Binguni, na kuboresha huduma katika Hospitali ya Mnazi Mmoja. SOMA: Rais Mwinyi amuapisha Mwanasheria Mkuu Zanzibar

Kwa upande wa elimu, Rais Mwinyi alisema Serikali itajenga madarasa 2,000, shule tatu za sekondari za wasichana kwa kila mkoa, chuo cha ualimu cha kisasa, na kuajiri walimu 7,691. Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha utumishi wa umma kwa kuboresha mafunzo, maslahi na nidhamu ya kazi, huku taasisi za ZAECA na CAG zikiimarisha udhibiti wa matumizi ya fedha za umma.

Akizungumzia Uchumi wa Buluu, Rais Mwinyi amesema Serikali inalenga kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa kutoka 800,000 hadi 1,500,000 kwa mwaka, na kuongeza uzalishaji wa mwani mkavu hadi tani 40,000 ifikapo mwaka 2030. Vilevile, Serikali itatekeleza miradi ya uvuvi na kilimo cha mwani, kujenga madiko, masoko ya samaki, na kuwawezesha wavuvi kwa njia za kibiashara.

Kwa upande wa usafiri wa anga, Rais Mwinyi alisema Serikali imelenga kuongeza idadi ya abiria wa ndege, kujenga vituo vya mafuta, karakana ya matengenezo, na jengo jipya la abiria Pemba, sambamba na uboreshaji wa barabara ya kurukia ndege.

Serikali pia itaendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 100, mafunzo ya ujasiriamali, na kutekeleza mpango maalum wa vijana wabunifu utakaosaidia kuzalisha ajira 350,000 mpya.

Rais Mwinyi alihitimisha kwa kusisitiza dhamira ya Serikali kulinda ustawi wa wanawake, watoto, wazee na watu wenye mahitaji maalum, sambamba na kukamilisha ujenzi wa nyumba 4,715 katika maeneo ya Chumbuni, Nyamanzi, Kisakasaka na Pemba.

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button