Amani ya nchi yatakiwa kuendelezwa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wananchi kwa ujumla kuendelea kuiombea nchi amani na kudumisha mshikamano wa kijamii.

Akizungumza leo, 21 Novemba 2025, mara baada ya kujumuika na Waumini katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika Masjid Rashidin, Dole Sokoni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk. Mwinyi alisema kila mwananchi ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuhimiza na kukumbusha umuhimu wa amani nchini.

“Ni neema kubwa kuona amani imedumu kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Hii inapaswa kuendelezwa kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuendeleza dua na ibada,” alisema Rais Mwinyi. SOMA: Rais Mwinyi awateua makatibu wakuu

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema kuwa kuwepo kwa amani kunaiwezesha nchi kutekeleza kikamilifu mipango ya maendeleo katika nyanja mbalimbali. Aliongeza kuunga mkono tangazo la siku ya Jumatatu, 24 Novemba 2025, kuwa siku maalum ya Waumini kufunga na kuiombea nchi amani.

Rais Mwinyi pia alibainisha madhara makubwa yanayoweza kutokea kutokana na kukosekana kwa amani, yakiwemo kupungua kwa upatikanaji wa chakula, kupanda kwa bei za bidhaa, na kuongezeka kwa misukosuko ya kijamii.

Aidha, aliwataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea dua viongozi wakuu wa serikali ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kufanikisha ahadi zao kwa wananchi.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting websiteMore Details For Us→→   http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button