Rais Salva Kiir awafuta kazi mawaziri wawili

RAIS wa Sudan Kusini, Salva Kiir amewafuta kazi mawaziri wawili na gavana wa jimbo la Warrap kaskazini mwa nchi hiyo.
–
Kiir alimfukuza kazi Waziri wa Maswala ya Rais, Barnaba Marial Benjamin, pamoja na Waziri wa Biashara, Kuol Athian.
–
Pia alimuondoa Waziri wa Utumishi wa Umma, Bangasi Joseph Bakosoro na kumfanya Waziri wa Masuala ya Rais.
–
Hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kazi, lakini ni kufuatia kutimuliwa hivi karibuni kwa maofisa kadhaa wa usalama ikiwa ni pamoja na mkuu wa polisi kutokana na uvumi wa mapinduzi.



