Rais Samia Suluhu Hassan akisafiri kwa treni ya SGR kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ambapo pamoja na majukumu mengine pia atashiriki zoezi la uboreshaji wa taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura leo Mei 17 katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji, Chamwino mkoani Dodoma. (Picha na Ikulu)