Rais Samia ampeleka Prof Janabi MNH, ateua bosi mpya JKCI

Profesa Mohamed Yakubi Janabi

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Moyo yya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Yakubi Janabi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Profesa Janabi anachukua nafasi ya Profesa Lawrence Maseru ambaye amestaafu.

Pia amemteua Dk Peter Kisenge kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Dk Kisenge ni Mkurugenzi wa Tafiti na Mafunzo JKCI.

Advertisement

Taarifa ya Ikulu imesema uteuzi huo unaanza Oktoba 2.