Rais Samia amuomboleza mwanamuziki Steven Hiza

Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, kufuatia kifo cha mwanamuziki mkongwe, Steven Hiza.

Hiza amefariki jana jioni nyumbani kwake, jijini Tanga.

Taarifa ya Ikulu imesema Rais Samia amemtaja Marehemu Hiza kuwa msanii mahiri na mzalendo aliyetumia kipaji chake kuelimisha, kuburudisha na kuhamasisha jamii, huku akitumia sanaa kama chombo cha kuimarisha maadili, umoja na utambulisho wa Taifa.

Marehemu, aliyewahi kuhudumu katika bendi ya muziki ya Atomic Jazz Band, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza na kuendeleza muziki wa Tanzania, hususan kupitia wimbo wake maarufu wa “Tanzania Yetu ndiyo Nchi ya Furaha,” wenye hisia za uzalendo na mshikamano wa kitaifa.

Vilevile, Rais Samia ametoa rai kwa wanamuziki na wadau wa tasnia ya muziki nchini kudumisha na kuenzi mchango wake kwa kuendeleza misingi ya uzalendo, ubunifu na uzalishaji wa kazi za sanaa zenye tija kwa Taifa.

Rais Samia anatoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa, wanamuziki, wadau wa sanaa na Watanzania wote kwa ujumla.

Aidha, anawaombea wafiwa uvumilivu, faraja na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba, huku akimuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Steven Hiza mahali pema peponi, Amina.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. These best thc gummies to relax were expressly the amicable of outcome that works expressively suitable a nighttime routine. The flavor was teeming, not too chocolate, and there wasn’t any strange hemp-heavy taste hanging far afterward. They also satisfy perfectly as put one’s feet up gummies because the blanket vibe felt calm and easygoing. As anyone browsing sleep gummies, this well-wishing of yield makes intuition too because it pairs at the end of the day grammatically with a quietness evening, a silver screen, or upstanding slowing things down at the end of the day.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button