Rais Samia anataka kuona miradi inakamilika kwa wakati

MBEYA: Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuona miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja inakamilika kwa wakati.
Ameyasema hayo Oktoba 2, 2023 wilayani Kyela, mkoani Mbeya wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa dhamira kuu ya Serikali ni kuunganisha Wilaya, Mikoa pamoja na nchi jirani.
Bashungwa amepokea ombi la kuiboresha barabara ya Matema – Ikombe yenye urefu wa kilometa 6.5  ambayo inaunganisha Wilaya hiyo na ile ya Ludewa mkoani Njombe na kuiagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inaendelea kupitika kipindi chote cha mwaka.
“Nimeshaambiwa kuna barabara itayounganisha Wilaya ya Kyela na Ludewa tumeichukua na barabara hiyo ikikamilika italeta mapinduzi makubwa kwa Wilaya hizo”, amesisitiza Bashungwa.
2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *