RAIS Dk Samia Suluhu Hassan ametoa ppole kufuatia kifo cha mtangazaji Wasafi Media Group, Khadija Shaibu (Dida)
Kupitia ukurasa wake wa X Rais Samia ameandika: “Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wasafi Media Group kwa kuondokewa na ndugu yetu, Khadija Shaibu (Dida).
Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma awape subra. Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwa hakika kwake Yeye tutarejea.”
Wasafi Media Group imetangaza kifo cha Dida Oktoba 4.