Rais Samia ateua wenyeviti TARI, NIT

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), anajaza nafasi ya Dk Tausi Kida aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Uwekezaji.

Aidha, Rais Samia amemteua Profesa Ulingeta Obadia Lebson Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa kipindi cha miaka mitatu (03).

Prof. Mbamba anachukua nafasi ya Prof.

Blasius Bavo Nyichomba ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 5, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa uteuzi wa Mwenyekiti Bodi ya TARI, umeanza Aprili 2, 2023 na Mwenyekiti Baraza la NIT umeanza Machi 29, 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button