Rais Samia awapa neno wanafunzi darasa la saba

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewatakia heri wanafunzi wote wa Darasa la Saba wanaoanza mitihani yao ya kuhitimu leo.

“Mmefikia hatua muhimu ya safari yenu ya awali, kuelekea njia mtakazochagua siku za usoni katika kutoa mchango wenu kusukumu mbele gurudumu la maendeleo ya Taifa letu.” amesema Rais Samia.

.”Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu aliyewasimamia toka mwanzo wa safari hii ya elimu hadi sasa, akawape utulivu na afya njema, ili mfanye vizuri mitihani yenu.” ameongeza

Ameswma Serikali tayari imekamilisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wote mtakaoendelea na kidato cha kwanza mwaka 2024.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button