Rais Samia azindua jengo la Halmashauri Bumbuli

TANGA: RAIS Samia Suluhu Hassan amezindua jengo jipya la Halmashauri ya Bumbuli, mkoani Tanga, akisisitiza umuhimu wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 24, 2025 katika wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga, mara baada ya kuzindua jengo hilo, Rais Samia ameeleza furaha yake kwa kupokelewa vizuri na wananchi wa Bumbuli wakiongozwa na Mbunge wao January Makamba akisema amefurahi pia kuona mabango ya upendo kutoka kwa wananchi ambayo yanayosomeka: “Tunakupenda sana Mama.”

Rais Samia amewashukuru wakandarasi, washauri, na wafanyakazi wa Halmashauri kwa juhudi zao katika kuhakikisha jengo linakamilika kwa ubora, akisema kuwa kazi yao ni mfano mzuri wa ushirikiano wa kiutendaji.

Vilevile ameeleza kuwa, jengo hilo limejengwa kwa lengo la kuhakikisha watumishi wa Halmashauri wanafanya kazi katika mazingira bora na wananchi wanapata huduma kwa urahisi.

“Jengo hili ni la wananchi wa Bumbuli. Huduma zote zitapatikana hapa, na naomba mlitumie kwa manufaa yenu. Lengo letu ni kuboresha huduma kwa wananchi na kutoa fursa kwa watumishi wetu kufanya kazi zao kwa ufanisi,” amesema Rais Samia.

Kwa uzinduzi huu, Rais Samia amekazia dhamira yake ya kuhakikisha maendeleo yanaendelea kusogea kwa kasi na wananchi wanapata huduma bora karibu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button